Benki Ya Dunia Yaahidi Kuunga Mkono Hustler Fund
Rais William Ruto amekaribisha hatua ya Benki ya Dunia kuunga mkono mfuko wa ukopaji Hustler Fund, katika kuwanusuru walio hatarini katika jamii.
Haya yanajiri baada ya Mkuu wa Nchi kufanya mkutano katika Ikulu na wajumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Victoria Kwakwa jana Jumanne katika Ikulu ya Nairobi.
Rais ruto amesema usaidizi wa kiufundi kutoka kwa Benki ya Dunia utasaidia pakubwa katika kufanya hazina hiyo kuwajumuishi zaidi na kuleta mabadiliko kwa mamilioni ya Wakenya wa kawaida.
Kwa upande wake, Kwakwa alikubali ajenda ya Benki inayoendelea ya kukabiliana na hali ya hewa ambayo inategemea ukame uliopo.
Serikali imedhamiria kukagua historia ya kukopa ya karibu wateja milioni sita ili kuwawezesha kupata pesa zaidi.
Rais William Ruto amesema Hustler Fund itapitia historia ya kukopa ya watumiaji milioni 18 kila baada ya miezi minne na kuwatunuku daraja la kifedha.
Aidha rais ruto amefafanua kuwa daraja la fedha ndilo litakaloamua ukomo wa mkopo wao kulingana na jinsi wanavyokopa na kurejesha mara kwa mara.
Rais pia ametangaza kuzindua bidhaa mpya, Hustler Fund Micro Credit, itakayoruhusu saccos na vikundi kukopa kwa niaba ya wanachama wao.