Home » TSC Yaelezea Uhamisho Wa Walimu Wakuu Kisii

Siku chache baada ya maswali kuibuka kuhusu uaminifu wa matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KSCE, haswa katika eneo la Kisii, Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) imehamisha walimu wakuu kwa wingi kutoka eneo hilo.

 

Kulingana na ripoti, wakuu wa shule waliohamishwa walikuwa kutoka shule za ngazi za kaunti na za ziada kutoka Kisii ambazo ziliandikisha matokeo ya kushangaza.

 

Wakati TSC ikielezea uhamishaji huo, tume imebaini kuwa lilikuwa ni zoezi la kawaida linalolenga kufikia mgawanyo sawa na matumizi bora ya rasilimali.

 

Kwa mfano, mwalimu mkuu Chrispinus Owino wa Kadinali Otunga- ambaye shule yake ilipata alama 10.26 katika mtihani wa (KCSE) 2022 – amehamishwa hadi Shule ya Upili ya Wavulana ya St Peter’s Mumias, Kaunti ya Kakamega.

 

Nafasi ya Owino imechukuliwa na Albert Ombiro, ambaye awali aliiongoza St Paul’s Gekano Boys.

 

Boniface Masese, ambaye amechangia shule ya Upili ya Igonga D.O.K kufikia viwango vipya baada ya kupata wastani ya alama 10.24 katika mitihani ya KCSE ya 2022, pia amehamishiwa Shule ya Upili ya Bishop Mugendi Nyakegogi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Masese amethibitisha kuwa yuko tayari kuiga mafanikio katika shule nyingine.

 

Uhamisho huo wa walimu wengi unajiri huku kukiwa na madai ya ukiukaji wa taratibu za mitihani, wengi wao wakihoji uhalali wa matokeo hayo kutoka sehemu za nchi.

 

Madai hayo, hata hivyo, yamekataliwa na waziri wa Elimu Ezekiel Machogu ambaye amebainisha kuwa madai hayo ya upendeleo yanaweza kuhusishwa na kupigwa marufuku kwa uorodheshaji huo jambo ambalo TSC imekanusha.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!