Home » Rais Ruto Kukutana Na Magavana

Rais William Ruto anatarajiwa kukutana na magavana wiki hii ili kumaliza mzozo kuhusu mgao wa fedha za kaunti.

 

Mkutano huo unaowaleta pamoja afisi ya urais na magavana, unajiri baada ya mkutano ulioongozwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua kukosa kufikia mwafaka.

 

Baraza la Magavana linashikilia msimamo wake kwamba mgao sawa uongezwe hadi Shilingi bilioni  425 kutoka Shilingi bilioni 370 zilizopendekezwa kwa mwaka wa kifedha wa 2022/23.

Magavana wanasema wanatumai mkutano na Rais Ruto utasaidia kumaliza mkwamo huo.

 

Hazina ya Kitaifa inasema inaweza tu kuongeza kiasi hicho hadi Shilingi bilioni 380 huku Tume ya Ugavi wa Mapato (CRA) ikitaka mgao wa Shilingi bilioni  470.

 

CRA inasema pendekezo lake limetayarishwa dhidi ya hali ya nyuma ya kufufua uchumi wa nchi kufuatia kuzuiliwa kwa homa tandavu la korona.

 

CRA imeagizwa na Katiba kutoa mapendekezo kwa msingi wa ugawaji sawa wa mapato yanayotolewa na serikali ya kitaifa na kaunti.

 

Aidha, tume inatakiwa kutoa mapendekezo miezi sita kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha au baadaye iliyokubaliwa kati ya Hazina na CRA.

 

Naibu rais rigathi Gachagua, ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Bajeti ya Serikali na Uchumi (IBEC), alisema kaunti hazipaswi kutarajia pesa zozote kupita walizozungumzia awali.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!