Home » Hospitali ya Meru Yazika miili 153 Ambayo Haijadaiwa

Hospitali ya Meru Yazika miili 153 Ambayo Haijadaiwa

Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Meru imezika miili 153 ambayo haijadaiwa katika makaburi baada ya chumba chake cha kuhifadhia maiti kuripotiwa kujaa kupita kiasi.

 

Afisa wa afya wa hospitali hiyo Misheck Nyingi, akizungumza na Mwanahabari baada ya shughuli hiyo iliyoanza leo hii Jumamosi asubuhi, amesema miili hiyo kati yao ilikuwa ya watoto 111 na watu wazima 42.

 

Kulingana na Nyingi, mingi wa miili hiyo ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo na polisi, na walilazimika kuizika baada ya kupata uamuzi kutoka kwa mahakamani

 

Aidha, amedai kuwa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo bado kimesalia na miili mia 165 ambayo haijadaiwa, 40 kati yake watakuwa wakitafuta amri ya mahakama ya kutupwa wiki ijayo.

 

Afisa huyo amesema hospitali hiyo inaandaa sera ambapo watashirikiana na wasimamizi, Machifu, na wana-usalama husika ili kuhakikisha kuwa utambulisho wa miili inayoletwa na polisi katika siku za usoni inaanzishwa ili kuepusha mzigo tena kwenye chumba cha maiti.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!