Kesi ya Mauaji ya Geoffrey Otieno Yahairishwa

Kesi ya mauaji dhidi ya Geoffrey Otieno Okuto, aliyekuwa mlinzi wa Waziri wa Jinsia na Utumishi wa Umma Aisha Jumwa, kuhusu mauaji ya mfuasi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) imeharishwa hadi Juni 5.
Aidha itakuwa mara ya kwanza Otieno kukabiliwa na mashahidi pekee yake kuhusu kupigwa risasi kwa Jola Ngumbao mnamo 2019, baada ya shtaka dhidi ya mshtakiwa mwenzake, waziri Jumwa, kufutiliwa mbali.
Wawili hao awali walishtakiwa pamoja kuhusu mauaji ya Ngumbao wakati wa uchaguzi mdogo wa Malindi, lakini wakati huo aliyekuwa mbunge wa malindi ambaye kwa sasa ni waziri wa jinsia Jumwa aliachiliwa baada ya ushahidi mpya kama ulivyokaguliwa na serikali na kumwondolea mashtaka.
Mahakama ilikuwa imeambiwa kuwa wawili hao na wafuasi wao walivamia nyumba ya Reuben Katana ambapo mkutano wa mkakati wa ODM ulikuwa ukiendelea, na kusababisha kuuawa kwa Ngumbao.
Mnamo Desemba mwaka jana, Mahakama Kuu ilimwachilia huru waziri Jumwa kutoka kwa kesi ya mauaji, na kukanusha kuwa bado anaweza kukamatwa na kushtakiwa katika siku zijazo.
Kulingan na Jaji wa Mahakama Kuu ya Mombasa Ann Ong’injo alimwachilia Jumwa kufuatia Kifungu cha 87(a) cha Sheria ya Mwenendo wa Uhalifu.
Kifungu hicho kinaeleza kuwa upande wa mashtaka unaweza, kwa ridhaa ya mahakama, au kwa maelekezo ya Mkurugenzi wa Mashtaka, wakati wowote kabla ya hukumu kutolewa, kujitoa katika mashtaka ya mtu yeyote, na baada ya kujitoa, iwapo itatolewa kabla ya mtuhumiwa kuitwa kujitetea ataachiliwa lakini kuachiliwa kwa mtuhumiwa hakutakuwa kama kizuizi kwa kesi zinazofuata dhidi yake kwa sababu ya ukweli uo huo.