Home » Serikali Kutenga Ksh Bilioni 5 Kwa Maabara za Shule Za Junior Secondary

Serikali Kutenga Ksh Bilioni 5 Kwa Maabara za Shule Za Junior Secondary

Serikali itawekeza angalau shilingi bilioni 5  kuelekeza kwa vifaa vya ujenzi ili kuanzisha maabara katika Shule za junior secondary (JSS).

Katibu Mkuu wa Elimu Belio Kipsang anasema hii ni katika juhudi za kuhakikisha miundomsingi ya kutosha huku akiwahakikishia wazazi kwamba kuna vifaa vya kutosha vya kujifunzia kwa wanafunzi milioni 1.2 wanaoingia kwenye Mtaala unaozingatia Umahiri CBC.

Akizungumza katika Shule ya Msingi ya Arap Moi mjini Kajiado alipofuatilia kuripoti kwa wanafunzi wa JSS, Kipsang amesema washikadau wa elimu wanapaswa kufanya kazi bega kwa bega kuwatayarisha wanafunzi hao kuchagua njia katika ngazi ya shule za upili.

Aidha, amewataka wazazi kuacha hofu juu ya mabadiliko hayo, akisema ilikusudiwa tu kufuatilia na kutathmini maendeleo ya wanafunzi.

Kulingana na katibu Kipsang, wizara ya elimu inashirikiana kwa karibu na Wabunge kuwataka pia kutumia sehemu ya pesa za maendeleo ya maeneobunge NG-CDF katika kuboresha miundombinu ya shule.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!