Home » Wamalwa: Azimio Haitaki ”Handshake” Tunapinga Ukabila

Wamalwa: Azimio Haitaki ”Handshake” Tunapinga Ukabila

Eugene Wamalwa

Aliyekuwa waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa amedai kuwa sababu kuu ya mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na muungano wa Azimio la Umoja ni kupiga vita ukabila na wala sio kulazimisha kupeana mkono (Handshake) na serikali kama wanavyodai wengi.

 

Kulingana na Wamalwa, Rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua wamekuwa wakitenga sehemu kubwa ya nafasi za serikali kwa watu kutoka makabila yao na kuwapa Wakenya wachache waliosalia kutoka makabila mengine.

 

Wamalwa amesema kuwa kuna haja ya kuwa na serikali ambayo inawateua Wakenya kwa usawa katika nyadhifa za serikali zisizo na makabila yao.

 

Mshirika huyo wa Azimio amebainisha kuwa kinara wa muungano huo Raila Odinga atashughulikia masuala mbalimbali yaliyotajwa na wafuasi wake leo katika mkutano unaoendela katika uwanja wa Jacaranda .
Wamalwa ameongezea kuwa mkutano huo utakuwa wa amani na wa kutafuta kusikiliza matatizo yanayowasumbua Wakenya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!