Home » Bahati Adokeza Kufanya Collabo Na Harmonize

Msanii kelvin kioko almaaruf Bahati kenya anaendelea kutikisa kila upande kimuziki na hata kutokea kufanya collabo zilizokubalika miongoni mwa mashabiki wake.

Wakati Bahati bado anaendelea kufanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Nowe Sweety,’ ameonyesha kuwa hataki kulaza damu kwenye muziki, ametangaza ujio wa kazi yake mpya na msanii wa BongoFleva Harmonize.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bahati amepostI picha akiwa na Harmonize na kuandika ‘2023 are You Ready for Us??? Brother @Harmonize_tz ‘ na Harmonize akajibu kwa kuandika ‘SEND IT BRO I HAVE ONLY ONE WATSP NUMBER LOVE YOU NO MARA WAA !!! GETO BOYS”

Iwapo Bahati atafanikiwa kuachia wimbo wake na Harmonize atakuwa ameongeza orodha ya wasanii wa Bongofleva aliofanya nao kazi ikizingatiwa kuwa ana kazi ya pamoja na Rayvanny, Mbosso na Aslay.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!