Home » MCK Yarejelea Kadi Za Wanahabari Kuwakamata Wanahabari Bandia

MCK Yarejelea Kadi Za Wanahabari Kuwakamata Wanahabari Bandia

Baraza la vyombo vya habari nchini (MCK) limeazimia kurudisha kadi zote za idhini za wanahabari ili kutokuwa na walaghai wanaojifanya wanahabari.

Katika taarifa yake baraza hilo limesema litatoa kadi mpya za vyombo vya habari zenye vipengele vya ziada ambavyo vitarahisisha kuidhinisha kadi hiyo kwa kutumia simu yoyote ya kisasa.

Uidhinishaji husaidia wanahabari kupata habari kwa kuruhusu ushiriki katika makongamano, warsha, mafunzo na mikusanyiko mingine.
Pia huongeza ulinzi wa haki na marupurupu ya wanahabari katika kutekeleza majukumu yao.

Kulingana na MCK, baadhi ya kadi zinastahiki kuidhinishwa. Waandishi wa habari wanaofanya kazi katika makampuni ya vyombo vya habari, waandishi wa kujitegemea, waandishi wa habari wa nchi za kigeni,, wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari na makampuni ya Utangazaji na Wakufunzi wake.

Wanahabari wote wanaotaka kuidhinishwa na MCK, wanatakiwa kutoa barua kutoka kwa mwajiri, shahada halisi au cheti cha diploma katika mawasiliano kutoka kwa taasisi inayotambulika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!