Home » Chameleone Kubuni Bendi Ya Muziki Ya Familia

Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amefichua mpango wa kuunda bendi ya familia itakayojumuisha ndugu zake, Pallaso na Weasel.

Katika mahojiano hivi karibuni, Chameleone ameeleza kuwa watatu hao bado wapo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kufikia makubaliano.
Bendi hiyo huenda ikazinduliwa hivi karibuni katika hafla itakayofanyika jijini Kampala, katika uwanja wa Namboole.

“Tunapanga kuanzisha bendi ya familia na tutatoa mwelekeo hivi karibuni. Uzinduzi huo unahitaji ukumbi mkubwa ambao hauko tayari kwa sasa. Tunataka eneo ambalo linaweza kuchukua zaidi ya watu 40, 000,” alisema.

Jose Chameleone ameweka wazi hayo kwenye mkao na waandishi wa habari wakati akielezea mipango yake juu tamasha lake “Gwanga Mujje” litakalofanyika huko Lugogo Cricket Oval mwezi Februari mwaka huu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!