Home » Mwanaume Amuuwa Mtoto Wake Wa Kambo Uasin Gishu

Polisi huko Turbo, Kaunti ya Uasin Gishu wameanzisha msako wa kumsaka mwanamume anayedaiwa kumuua mtoto wake wa kambo wa wiki moja Jana jioni.

Daniel Kipchumba anasemekana kumdanganya mkewe kwenda nje ya nyumba ili kuomba usaidizi baada ya kujifanya kuugua maradhi ambayo hakuyataja mwendo wa kumi na mbili asubuhi ya jana.

Ripoti ya polisi iliyotolewa imesema Kipchumba alioana na mkewe wa miaka 12, Grace Atwoli, mnamo Desemba mwaka jana baada ya kutengana 2019.

Wakati huo alikuwa mjamzito sana kutokana na uhusiano na mwanamume mwingine.

Inasemekana kwamba Kipchumba alimwambia mkewe kwamba alikuwa akijisikia vibaya na akamwomba amwite mamake kumsaidia kumpeleka hospitali.

Grace aliporudi baada ya kumwita mamake ili kumsaidia kipchumba kwenda hosptalini hakupatikana mumewe.

Wawili hao walikutana na maiti ya mtoto huyo mwenye umri wa wiki moja ikiwa imelala kwenye godoro ikiwa na alama zinazoonekana shingoni, damu kutapakaa kila sehemu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!