Home » Mwanamke Ashtakiwa Narok Kwa Kunajisi Mvulana Wa Miaka 15

Mwanamke Ashtakiwa Narok Kwa Kunajisi Mvulana Wa Miaka 15

Mwanamke mmoja huko Narok ameshtakiwa kwa madai ya kumnajisi mvulana wa umri wa miaka 15, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili.

Akifikishwa mbele ya Hakimu Rosalinda Shinyanda, mahakama hiyo imeambiwa kwamba Mary Njoki alidaiwa kutekeleza uhalifu huo mnamo Januari 4,2023 katika mtaa wa Fanaka viungani mwa Narok.

Mshukiwa huyo anasemekana kumnajisi mtoto huyo na pia kumshika sehemu zake za siri vibaya.

Mwendesha mashtaka ameiomba mahakama kumnyima mshukiwa dhamana kwa madai kuwa yeye ni jamaa wa mtoto huyo na huenda mzozo ukazuka kati yake na mtoto wa mtoto huyo.

Aidha Upande wa mashtaka pia umeiomba mahakama kuharakisha upelelezi na uamuzi ili kuwapa wazazi nafasi ya kuwasilisha ushahidi.

Katika mahakama hiyo mwanaume mmoja alishtakiwa kwa kosa la kujihusisha na uuzaji wa nyama ambazo zinatokana na wanyama pori bila kuwa na leseni jambo ambalo ni kinyume cha katiba kwa mujibu wa kifungu cha 98(1) cha uhifadhi wa wanyamapori cha mwaka 2013.

Konene Sordo alinaswa na kilo mia 170 za nyama ya pundamilia mnamo Januari 10, 2023 huko Septai Narok Kusini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!