Home » Naibu Gavana Wa Machakos Amsuta Mbunge Wa Machakos

Naibu Gavana Wa Machakos Amsuta Mbunge Wa Machakos

Naibu Gavana wa Machakos Francis Mwangangi amemsuta Mbunge wa Machakos Mjini Caleb Mule kwa kukashifu uteuzi wa gavana Wavinya Ndeti wa Maafisa Wakuu.

Akiwahutubia wakaazi wa eneo bunge la Machakos Mjini, Mwangangi alimkashifu mbunge wa eneo hilo kwa kuzua vita dhidi ya orodha ya Wavinya wiki iliyopita.

Mbunge Caleb Mule amekuwa akimshutumu Wavinya kwa kutoa kazi zenye faida kwa wasio wakaazi kwa gharama ya wenyeji.

Lakini naibu gavana huyo alibainisha kuwa Machakos ni kaunti ya watu wote nchini ambayo inahitaji kuhudumia jamii nyingine katika usambazaji wa nafasi za kazi zilizopo.

Pia aliunga mkono wito wa Rais William Ruto wa kutaka tume ya uchunguzi iundwe kuchunguza njama za kugeuza maamuzi ya wakenya katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!