Home » Jeremiah Kioni Adai Muungano Wa Azimio Ulishinda Uchaguzi Mwaka Jana

Jeremiah Kioni Adai Muungano Wa Azimio Ulishinda Uchaguzi Mwaka Jana


Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya kwa mara nyingine umejitokeza kusema kuwa mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9, mwaka jana Raila Odinga, alishinda kinyang’anyiro hicho dhidi ya mshindani wake wa wakati huo ambaye sasa ni rais, William Ruto.

Safari hii ikirejelea ripoti iliyotolewa na anayedaiwa kuwa mtoa siri ndani ya IEBC, Azimio imesema kuwa Raila alishinda uchaguzi huo baada ya kupata kura 8,170,355 mbele ya Ruto ambaye akisemekana kuwa na kura 5,919,973.

Akizungumza jijini Nairobi, Katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni amebainisha kuwa ripoti waliyopata kutoka kwa mfichua siri huyo, imethibitisha bila shaka kuwa Odinga ndiye aliibuka na ushindi katika kinyang’anyiro cha Agosti mwaka huu.

Kulingana na Kioni, ripoti hiyo inaonyesha kuwa matokeo ya kura kutoka maeneo bunge 144 yalidaiwa kubadilishwa na baadhi ya maafisa wa IEBC ili kumpa Ruto ushindi wa kinyang’anyiro hicho, na kwamba uchunguzi huo ulifanywa na kundi kwa jina Vanguard Africa.

Pia amedai makosa mengi yalifanyika katika eneo la Mlima Kenya ambalo lina kapu kubwa la wapiga kura.

Kioni aliongeza kuwa muungano wa Azimio utatoa ripoti ya kina kuhusu matokeo hayo, mara baada ya kiongozi wao Raila Odinga kurejea kutoka Afrika Kusini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!