Home » Bangi Yenye Thamani Ya Shilingi Milioni 2.3 Yapatikana Migori

Bangi Yenye Thamani Ya Shilingi Milioni 2.3 Yapatikana Migori

Polisi katika kaunti ndogo ya Kuria Magharibi  kaunti ya Migori wanamzuilia mshukiwa mmoja na kupata kilo 178 za bangi yenye thamani ya shilingi Milioni 2.355

Kamanda wa polisi eneo hilo Cleti Kimaiyo anasema bangi hiyo ilipatikana katika boma mbili tofauti wakati wa msako wa jioni ya jana  uliondeshwa na polisi baada ya kupokea taarifa kutoka kwa umma.

Katika oparesheni ya kwanza kwenye kijiji cha Bimaiti kata ndogo ya Ngochoni Kimaiyo, amesema walipata bangi yenye thamani ya shilling elfu 855.

Anasema katika oparesheni hiyo walifanikiwa kumkamata mshukiwa Thomas Nsoto mwenye umri wa miaka 34 kama mshukiwa mkuu na anazuiliwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani.

Katika msako wa pili uliofanyika katika kijiji cha Nyangiti polisi walifanikiwa kuopata magunia matano ya bangi yenye uzani wa kilo 150 na thamani ya mtaani ya shilling milioni  1.5 katika boma la Gibebe Jackson.

Bangi hiyo inahifadhiwa katika kituo cha polisi cha Isebania ili kutumika mahakamani kama ushahidi

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!