Home » King Kaka Ahimiza Wakenya Kushabikia Wanamichezo Wao Bila Kushinikizwa

King Kaka Ahimiza Wakenya Kushabikia Wanamichezo Wao Bila Kushinikizwa

Rapper King Kaka /photo courtesy/

Baada ya wikendi yenye mihemko tele hatimaye Rapa King Kaka ametoa changamoto kwa wakenya kuanza kuwashabikia wanamichezo wao badala ya kushawishiwa kufanya hivyo na watu wa mataifa ya nje.

Kupitia miitandao ya kijamii, King Kaka amesema ameshangzwa na namna wakenya walijitokeza kumshangilia mwanadondi wa Tanzania mandonga ‘Mtu Kazi’ ilhali kuna wana michezo wengi wanaofanya vizuri kwenye nyanja mbali mbali.

Hitmaker huyo wa “Wajinga Nyinyi” amewataka wakenya kuwa wazalendo kwani hawahitaji shinikizo kutoka kwa watu wa nje kuwafanya kufuatilia matukio mbali mbali ya michezo nchini.

Hata hivyo, wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na rapa huyo wakisema michezo nchini Kenya imekosa mvuto na mbwembwe kutokana na wawekezaji duni.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!