Home » ‘Acha Kunizungumzia Kila Unapohojiwa,’ Anerlisa Aambia Ben Pol

‘Acha Kunizungumzia Kila Unapohojiwa,’ Anerlisa Aambia Ben Pol

picha kwa hisani

Kichuna kutoka Kenya Anerlisa ambaye alikuwa mke wa msanii wa Bongo fleva Ben Pol, ameonyesha kutofurahishwa na kile ambacho alikizungumza Ben Pol kwenye mahojiano yake na Ayo Tv kuwa hajawahi kufurahishwa na ndoa yake na mrembo huyo.

Kupitia mtandao wake wa Instagram anashangaa ni kwanini Ben Pol kila siku amekuwa akiongea mambo mengi ili aonekane mbaya mbele ya umma.

https://mideyahdigital.co.ke/2023/01/14/viongozi-wa-kike-baringo-wataka-serikali-kuingilia-kati-kukomesha-pombe-haramu/

“Ben, naona umenizoea na unachukulia ukimya wangu kama udhaifu wangu. Ulikuwa na uwezo wa kumwambia anaekuhoji asikuulize kuhusu mimi. Kwa nini unapenda kila mara mimi nionekane mbaya. Chini ya kapeti unanitumia jumbe tofauti tofauti na namna unavyoniongelea”, aliandika.

Pia amemtaka Ben Pol aache kumuongelea kwani ana mengi kumhusu ila amechagua kukaa kimya kama mwanamke.

https://mideyahdigital.co.ke/2023/01/14/mwakilishi-wadi-aitaka-wizara-ya-elimu-kuruhusu-wachezaji-kutumia-viwanja-vya-shule/

“Kama kweli wewe ni mwanaume, nakuomba uweke wazi jumbe zote ulizokuwa unanitumia tangu Desemba 25 hadi Januari 4, 2023. Nina mengi ya kuzungumza kuhusu wewe au kuonyesha, lakini nimechagua kusimama kama öwanamke,”alisema Anerlisa.

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!