Wizara ya Afya, kupitia Bodi ya Dawa na Sumu(PPB), imeonya Wakenya dhidi ya
kutumia vifaa vinavyozungumziwa sana nchini vya kupima DNA nyumbani
kwani vifaa hivyo havijaidhinishwa.
Haya yanajiri baada ya habari kuenea sana Kenya kwamba Wakenya sasa
wanaweza kukusanya chembechembe zao za DNA kwa uchunguzi wa nyumbani, huku
vifaa hivyo vikisemekana vinapatikana katika maduka mbali mbali ya dawa kwa
bei ya reja reja ya takriban Ksh.800.
Katika taarifa yake kwa vyumba vya habari hii leo,PPB imesema haijatoa mwanga
wa uuzaji wa vifaa hivyo vya majaribio, na kuwashauri Wakenya kuwa macho
na wauzaji wa rejareja hao.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa bodi hiyo Dkt. Fred Siyoi katika taarifa hiyo
amewataka Wateja kuripoti kwa PPB iwapo watakutana na muuzaji yeyote
anayeuza bidhaa zinazohusiana.