Home » “Simu Nyingi ni Ngono Nyingi” Aonya Justina Syokau!

Msanii Justina Syokau

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Justina Syokau amejitokeza na kuwaonya wanawake dhidi ya kupumbazwa na mapenzi ya mwanzo, akiwataka kujitathmini kwa undani iwapo kweli wanapendwa au ni ngono inayotafutwa kutoka kwao.

Katika mahojiano na mtangazaji wa runinga ya NTV Amina Abdi, Justina amedai kuwa ni tamaa ya ngono inayowafanya wanaume wengi kuwapigia wanawake simu mara kwa mara.

“Ninadhani wanaume wengine ni tamaa ya ngono inayowafanya wawapigie simu wanawake. Wasichana wanafaa kujiuliza, ukiona anakupigia sana simu, ni ngono anataka ama ni wewe anataka?” Justina alisema kwenye kipindi cha The Trend.

Hata hivyo Justina amesema kuwa wapo wanaume walio na nia nzuri wanapowatongoza na kuwachumbia wanawake japo ni adimu kuwapata.

“Lakini ninataka kusema kuwa kuna wanaume wazuri hata kama wanavutiwa na hilo, watabaki bado na hata kukuoa,” mwimbaji huyo aliongeza.

Justina alikuwa akisimulia ushuhuda wake kwa jinsi alivyojitunza kabla ya ndoa bila kushiriki tendo la ndoa na aliyekuwa mume wake lakini aliachwa tu baada ya hayo yote.

“Alikuwa mzuri sana. Alikuwa mzuri. Tulijihifadhi hadi ndoa. Tulikuwa na harusi safi. Sikujua siku moja anaweza niacha,” Justina alisema.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!