Home » Nakuru kukabiliana na vifo kutokana na Nyama ya Sumu!

Nakuru kukabiliana na vifo kutokana na Nyama ya Sumu!

Serikali ya kaunti ya Nakuru inatarajiwa kuanzisha mpango wa kutoa chanjo kwa mifugo katika eneo la Kuresoi  kuanzia kesho, hii ni baada ya mtu mmoja kuaga dunia na wengine kadhaa kuathirika baada ya kula nyama ya mzoga wa ng’ombe aliyechinjwa baada ya kufa.

Afisa mkuu idara ya mifugo na uvuvi  Daktari Michael Cheruiyot akitangaza mpango huu  amewarai wakaazi kuwa waangalifu na nyama wanayoitumia   ili kuzuia maradhi yanayosababishwa na bidhaa zinazotokona na wanyama.

Watu wawili tayari wameathirika katika maeneo ya Tinet na Kiptagich.

Wakat huo huo ametoa onyo dhidi ya wanaochinja na kuuza nyama  isiyoidhinishwa  na idara ya afya kukoma hara iwezekanavyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!