Home » Wakulima Wa Parachichi Wa Gatundu Wapata Hasara

Wakulima wa parachichi kutoka eneo bunge la Gatundu Kaskazini kaunti ya Kiambu wanahesabu hasara kubwa baada ya wezi kuanza kuvamia mashamba yao na kuvuna matunda hayo kinyume cha sheria.

 

Wezi hao wanaripotiwa kuvamia mashamba hayo majira ya usiku na kuvuna matunda hayo kwa ajili ya kuwauzia wafanyabiashara wa kati wanaonunua kwa bei ya kutupa na kuwaacha wakulima bila ya kuuza.

 

Wakulima wamekanusha uhalifu huo unaofanywa na wavulana kutoka vijiji mbalimbali ambao hupata hadi Sh3 kwa kipande cha parachichi kinachouzwa kwa wafanyabiashara wa kati ikilinganishwa na kati ya Sh 10-20 wanazofanya wanapouza matunda hayo kwa wauzaji bidhaa nje ya nchi wanaonunua kwa bei zao.

 

Wizi huo, walilalamikia kuwa unachangiwa na madalali walioongezeka wanaonunua matunda hayo ambayo vyanzo vyake havijulikani.
Wakulima hao walilalamika kwamba magenge yaliyojipanga ambayo yanapenya kwa kiasi kikubwa katika biashara ya parachichi yenye faida kubwa katika eneo hilo na kuwaibia mamia kwa maelfu ya matunda ya parachichi yanaweza kuwatumbukiza kwenye umaskini, kwa kuwa wanategemea matunda hayo kwa maisha yao.

 

Ongezeko la bei za matunda ya parachichi nchini na kimataifa pia limeripotiwa kuwavutia madalali wengi kwenye biashara hiyo.

 

Wakati wakulima hao wakifuraia kutokana na kushamiri kwa biashara ya parachichi, walisema kuibuka kwa wizi wa kupangwa unatishia matumaini yao yaliyopatikana baada ya biashara zao za kahawa na chai kuporomoka kutokana na kupenyezwa kwa sekta hizo na makampuni ya biashara.

 

Wakiongozwa na Peter Kabui Maina ambaye hivi majuzi alipoteza matunda ya parachichi ya thamani ya Sh250,000, wakulima hao walikashifu kuwa huenda wezi hao wakaishia kuzamisha sekta hiyo huku wakulima walioathirika wakifikiria kung’oa miti ya parachichi ili kujitosa katika biashara nyingine.

 

Kabui alibainisha kuwa vijiji vilivyoathiriwa zaidi katika eneo bunge hilo ni Turiru, Kariua, Mutuma, Mang’u, Mukuyuini miongoni mwa vingine ambapo wakulima sasa wanakosa usingizi usiku, wakiwa wamejihami kwa panga kulinda zao hilo dhidi ya wezi hao.

 

Joseph Waithaka, mzee wa kijiji cha Turiru, alitoa wito kwa serikali kuingilia kati haraka kwa kuimarisha usalama katika eneo hilo kupitia kuongezeka kwa doria za polisi na kuweka taa za usalama ili kupunguza uhalifu.

 

Wakulima hao wakati uo huo waliitaka serikali kutunga sheria zitakazowazuia madalali kuporomosha sekta hiyo ambayo mamilioni ya wakulima wanaitegemea ili kujikimu kiuchumi.

 

Kimani Gachuhi, kiongozi wa Gatundu Kaskazini alisema kuwa wakulima wengi katika eneo bunge hilo waliacha biashara ya kahawa na chai na kujitosa katika biashara ya parachichi ili kujikimu ili tu sekta hiyo ishuhudie wizi huo uliokithiri.

 

Gachihi alisikitika kuwa madalali wameanzisha maduka katika vijiji vyote wanakohifadhi matunda ya parachichi yaliyoibiwa na kuitaka serikali kuingilia kati ili kuwanusuru wakulima na hasara zaidi.

 

Sawa na jinsi serikali inavyopambana na makampuni ya kuuza kahawa na chai, kiongozi huyo wa eneo hilo alimtaka Naibu Rais Rigathi Gachagua kuingilia kati biashara ya parachichi ili kuokoa mamilioni ya wakulima wanaokabiliwa na umaskini na makampuni ya biashara.

 

Mahitaji ya parachichi katika soko la kimataifa yamekuwa yakiongezeka huku Kenya ikipata mabilioni ya mauzo ya nje.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!