Wakenya Wamsuta Naibu Rais Gachagua

Wakenya kwenye mitandao za kijamii wamemkashfu Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa matamshi ambaye alitoa kwa kwa Mawaziri waliochukizwa na uongozi wa Kenya kwanza kujiuzulu kufuatia agizo la Rais William Ruto kwa Tume ya Mishahara (SRC) kusitisha mapendekezo yao ya nyongeza ya mishahara.
Wakenya wwengi katika mitandao ya kijamii wanasema naibu rais anatumia nafais aliyonayo kukejeli wakenya wanaosaka ajira na hata baraza la mawaziri.
Akizungumza katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet wakati wa hafla ya kumshukuru Katibu Mkuu wa Hazina ya Kitaifa Chris Kiptoo, Gachagua alisisitiza utayari wa Rais William Ruto kuteua mawaziri mbadala walio tayari kukubali miundo iliyopo ya mishahara.
Naibu Rais alimsihi Rais Ruto kuelekeza fedha zilizopendekezwa ili kuimarisha sekta mbalimbali za uchumi, ikiwa ni pamoja na kununua mbolea ya ziada kwa wakulima.
Katika juhudi za kutetea uwajibikaji thabiti wa kifedha, Gachagua aliwaagiza watumishi wote wa ngazi za juu wa serikali kurejesha pesa za SRC endapo itapuuza maagizo ya Ruto.
Kurejesha pesa hizo pia kunaweza kukariri mbinu ya Ruto ya kukuza uwazi na uadilifu katika utawala wake.
Hata hivyo, alimuunga mkono Ruto, akiashiria kwamba watumishi wengine wa umma wanapaswa kupokea nyongeza za mishahara kuanzia Jumamosi, Julai 1.
Mawaziri wanatarajiwa kupokea Ksh1,056,000 kufikia Julai 2024 kutoka Ksh924,000 za sasa.
Mnamo Ijumaa, Juni 30, Ruto alikataa nyongeza ya mishahara ya asilimia 14 iliyopendekezwa na SRC. Badala yake, Mkuu wa Nchi aliielekeza tume hiyo kutoa hati za malipo zinazolingana kwa watumishi wote wa umma.