Home » Murkomen: Serikali Itahamisha Wachuuzi Kutoka Barabara Kuu

Murkomen: Serikali Itahamisha Wachuuzi Kutoka Barabara Kuu

Waziri wa Uchukuzi Kipuchumba Murkomen amesema kuwa serikali itahamisha wachuuzi na masoko ya wazi kutoka barabara kuu.

 

Waziri huyo alikuwa akizungumza huko Kericho, Londiani ambapo watu 52 wamethibitishwa kufariki huku watu wengine 35 wakipokea matibabu katika hospitali tofauti baada ya trela kugonga magari kadhaa katika makutano ya Londiani kwenye Barabara Kuu ya Kericho-Nakuru Ijumaa jioni.

 

Aidha Murkomen alisema kuwa Gavana wa Kericho Dkt Eric Mutai amejitolea kutafuta ardhi inayofaa kuhamisha soko hilo huku akiongeza kuwa atajenga barabara ya kufikia.

 

Ili kuepusha ajali nyingine katika eneo hilo, Murkomen alisema kuanzia Jumatatu, vizuizi vya mwendo kasi vitawekwa ili kupunguza kasi ya trafiki inayokuja kwenye barabara kuu.

 

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Londiani Agnes Kunga ambaye alizungumza na wahandishi wa habari kwa simu alisema polisi wanamsaka dereva wa trela ya Rwanda ambaye alitoweka baada ya ajali hiyo.

 

Wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao kando ya barabara wakiwemo waendesha boda boda pia walianguka kwenye ajali hiyo ya saa 6:30 usiku.

 

Naibu Gavana wa Kericho Fred Kirui alisema kuwa Kaunti ilituma ambulensi na maafisa wote wa matibabu kusaidia waathiriwa kwani mvua kubwa ilitatiza juhudi za uokoaji, huku kukiwa na msongamano mkubwa wa magari katika njia hiyo.

 

Wakenya wamefurika kwenye mitandao ya kijamii na jumbe za rambirambi kwa familia za waliofariki kwenye ajali hiyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!