Home » Atwoli Na Wenzake Kuapishwa

Jopo la kuwaajiri watu walioteuliwa wanaotaka kuchukua nafasi ya Noordi Haji kama Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma DPP limezinduliwa.

 

Kamati hiyo ya watu saba imeagizwa hii leo Jumanne kuwaruhusu kutekeleza zoezi hilo.

 

Wanachama wa jopo hilo ni pamoja na Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) Twalib Mbarak, na Wakili Mkuu Shadrack Mose.

 

Wengine ni Katibu Mkuu wa Utumishi wa Umma Mary Kimonye, Mary Adhiambo Maumga, Roseline Odede, na Richard Onsongo Bush Obwocha.

 

Jopo hilo sasa litateua mwenyekiti ambaye ataongoza timu katika uhakiki wa walioteuliwa.

 

Akiongoza hafla ya uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Anthony Muchiri ameitaka kamati hiyo kuzingatia uadilifu na haki katika mchakato wa uteuzi.

 

Haji aliteuliwa na Rais William Ruto kuwa mkuu mpya wa ujasusi NIS mnamo Mei 16, 2023, kabla ya kuchunguzwa na kuidhinishwa na Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mahusiano ya Kigeni mnamo Juni 13, 2023.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!