Home » Kindiki Atangaza Jumatano Sikukuu Ya Umma Kuadhimisha Eid-Ul-Adha

Kindiki Atangaza Jumatano Sikukuu Ya Umma Kuadhimisha Eid-Ul-Adha

Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki ametangaza Juni 28, 2023 kuwa sikukuu ya kuadhimisha Eid-Ul-Adha.

 

Kindiki amebainisha tangazo hilo katika notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa Jumatatu.

 

 

Eid-Ul-Adha kawaida huadhimishwa kwa siku tatu.

 

Iwapo itaanza machweo Jumatano, itaisha tarehe 1 Julai 2023.

 

Tamasha hilo ni ukumbusho wa ngano ya Kurani ya nia ya Nabii Ibrahim kumtoa dhabihu mwanawe Ismail kama kitendo cha utii kwa Mungu.

 

Waislamu wanaamini kwamba kabla ya kutekeleza dhabihu, Mungu alitoa kondoo badala ya Isamail. Katika simulizi ya Kikristo na Kiyahudi, Ibrahim anaamriwa kumuua mtoto mwingine, Isaka.

 

Wakati wa sikukuu, Uislamu hukumbuka kafara iliyotolewa na Ibrahimu kwa kuchinja wanyama na kuwasaidia masikini.

 

Likizo hiyo pia inajulikana kama Sikukuu ya Sadaka na huangukia mwishoni mwa Hija ya Kiislam ya kila mwaka ya Hajj (Ambapo maelfu humiminika Saudi Arabia kila mwaka kuzuru Makka eneo takatifu zaidi la Uislamu.)

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!