Homa Bay: Mwalimu Akamatwa Kwa Madai Ya Kumnajisi Mwanafunzi

Mwalimu wa shule ya upili mwenye umri wa miaka 29 amekamatwa kwa madai ya kumnajisi mwanafunzi wake wa kike mwenye umri wa miaka 16 katika Kaunti Ndogo ya Nhdiwa, Kaunti ya Homa Bay.
Mwalimu huyo anayefanya kazi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyamogo katika Kaunti Ndogo ya Ndhiwa, alikamatwa na maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Ndhiwa.
Mwalimu huyo anadaiwa kumnajisi msichana huyo kwa tarehe tofauti kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.
Inaripotiwa kuwa Mwalimu huyo anatumia keki kuwarubuni wasichana katika mahusiano ya kimapenzi.
Kulingana na babake mwathiriwa, aligundua kuwa msichana huyo alikuwa amenajisiwa na mwalimu huyo baada ya kuanza kuwa na dalili za ujauzito Kisha akawasiliana na polisi kuhakikisha mwalimu huyo amekamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Ndhiwa Paul Rioba alithibitisha kuwa mwalimu huyo kwa sasa yuko chini ya kizuizi kutokana na visa vingine vya unajisi.
Mwalimu huyo amezuiliwa katika Kituo cha Polisi Ndhiwa akisubiri kufikishwa mahakamani kwa kosa la kunajisi.