Home » Serikali Yabadilisha Tarehe Za Likizo Kwa Shule Zote

Serikali Yabadilisha Tarehe Za Likizo Kwa Shule Zote

Wizara ya Elimu hii leo Alhamisi imepanga upya tarehe za likizo ya muhula kuanza kutoka Jumanne, Juni 27, hadi Jumamosi, Julai 1, 2023.

 

Mabadiliko hayo yamefuatia ombi la wakuu wa shule chini ya Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari Kenya (KESSHA) kwa serikali kuhusiana masuala ya ndani.

 

Awali, wanafunzi wote katika shule za umma walipaswa kuenda kwa mapumziko ya muhula wa pili kuanzia Alhamisi, Juni 29, hadi Jumapili, Julai 2.

 

Katibu Mkuu wa Elimu Belio Kipsang aliwataka wasimamizi wa shule kuzingatia mabadiliko hayo.

 

Katika ombi la mwenyekiti wa KESSHA, Indimuli Kahi, aliomba mabadiliko hayo kwani tarehe ziliambatana na Kongamano la 46 la Kitaifa la chama hicho.

 

Kipsang alikariri umuhimu wa kongamano hilo, akibainisha kuwa unawaruhusu wasimamizi wa shule kukagua na kupendekeza mabadiliko katika uendeshaji wa shule.

 

Wizara ilitoa kalenda ya shule mnamo Januari 10, 2023, ikionyesha tarehe muhimu za mwaka wa masomo.

 

Muhula wa pili ulianza Mei 8, 2023, na utaendelea hadi Agosti 11, 2023.

 

Kisha wanafunzi watapumzika kwa likizo mnamo Agosti 12, 2023, kwa wiki mbili hadi Agosti 27, 2023.

 

Muhula wa tatu unatarajia kuanza Agosti 28, 2023, hadi Oktoba 27, 2023.

 

Baadaye, wanafunzi watapumzika kwa likizo ya muhula wa tatu kutoka Oktoba 28, 2023, hadi Januari 8, 2024 (kipindi cha wiki kumi).
Mitihani ya (KCPE) na Tathmini ya Elimu ya Shule ya Msingi ya Kenya (KPSEA) itaanza Oktoba 30, 2023, hadi Novemba 2, 2023.

 

Kwa upande mwingine, mtihani wa wanafunzi wa Sekondari kidato cha nne (KCSE) watafanya mitihani kuanzia Novemba 3, 2023 hadi Novemba 24, 2023. Usahihishaji utaanza baadaye Novemba 27, 2023 hadi Desemba 15, 2023.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!