Home » Waziri Kuria Amwonya Raila Baada Ya Rais Ruto Kumtetea

Saa chache baada ya Rais William Ruto kumtetea dhidi ya wapinzani kutokana na matamshi yake ya dharau dhidi ya wanahabari, Waziri wa Biashara Moses Kuria ameelekeza macho yake kwa muungano wa Azimio, ambao ulipinga Mswada wa Fedha wa 2023.

 

Huku Azimio ikitarajiwa kufanya kongamano la mazungumzo ya umma katika uwanja wa Kamukunji Jumanne, Juni 27, Kuria ameonya kuwa ataongoza maandamano ya kupinga kutatiza mipango ya upinzani.

 

Akizungumza na wanahabari, Karua ameeleza kuwa Raila na muungano wake wa Azimio la Umoja hawana uwezo wa kuandaa maandamano nchini kupinga Katiba akisema hatua hiyo ni kinyume cha sheria.

 

Aidha ameisuta Azimio kwa kujaribu kuwachochea wananchi badala ya kuandaa hoja zenye kujenga uchumi.

 

Mswada wa Fedha wa 2023 ulipendekeza mabadiliko kadhaa kwa sheria za ushuru nchini, ikijumuisha ongezeko la kiwango cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa bidhaa za petroli kutoka asilimia 8 hadi 16.

 

Kuria ametetea uamuzi wa serikali wa kuongeza ushuru wa VAT kwa bidhaa za petroli, akisema kuwa ongezeko la VAT litaongeza mapato na kupunguza nakisi ya bajeti.

 

Aidha Kuria anasema kuwa alipendezwa na mipango ya Rais William Ruto akimtetea dhidi ya wapinzani waliomshtumu kwa kutishia vyombo vya habari na kujaribu kushawishi sera za uchapishaji.

 

Mnamo Jumapili, Juni 18, Kuria alizua ghadhabu baada ya kushambulia Nation Media Group kwa kile alichodai kuwa ni utangazaji wa upendeleo wa Azimio la umoja.

 

Muungano wa Wanahabari wa Kenya (KUJ), Baraza la Vyombo vya Habari Kenya (MCK) na upinzani walimshinikiza Ruto kujitenga na matamshi tatanishi ya Kuria.

 

Hata hivyo, Ruto, mnamo Jumatano, Juni 21, aliteta kuwa Kuria alikuwa huru kutoa maoni yake, lakini serikali pia ilikuwa na wajibu wa kuendeleza uhuru wa vyombo vya habari jinsi ulivyokita mizizi katika Katiba.

 

Kuria Biashara alitetea ushauri wake na kueleza kwa nini alimtaka waziri wa hazina ya kitaifa Profesa Njuguna Ndung’u kufikiria kuondoa ushuru wa asilimia 35 kwa mafuta ya kula na badala yake kuweka asilimia 10 ya ushuru wa kukuza mauzo ya nje na uwekezaji.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!