Home » Siaya: Mchimba Dhahabu Afariki Baada Ya Mgodi Kuporomoka

Siaya: Mchimba Dhahabu Afariki Baada Ya Mgodi Kuporomoka

Mchimba dhahabu alifariki huku wengine watano wakiokolewa baada ya shimo la kuchimba madini kuporomoka katika kijiji cha Rarieda Uyore huko Alego-Usonga, Kaunti ya Siaya, Jumatatu usiku.

 

Mchimbaji huyo alikuwa pamoja na wenzake sita wakati wa msafara wao wa kawaida wa uchimbaji madini wakati shimo lilipoporomoka na kuwafunikwa wakiwa hai usiku wa manane.

 

Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Siaya, Benedict Mwangangi, watano hao waliokolewa mara moja na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Siaya ambapo watatu walitibiwa na kuruhusiwa.

 

Alisema wachimbaji wawili waliookolewa bado wanaendelea na matibabu katika kituo hicho huku akibainisha kuwa hali zao zinaendelea vizuri.

 

 

Mwili wa mchimba mgodi aliyefariki umechukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Siaya kusubiri kufanyiwa uchunguzi.

 

Mwangangi alisema uchunguzi unaendelea kubaini iwapo mgodi huo wa dhahabu ulikuwa unafanya kazi kihalali.

 

Wakati uo huo alitoa onyo kali kwa wachimbaji dhahabu sio tu katika kijiji cha Rarieda Uyore lakini kote Kaunti ya Siaya kuacha kuingia kwenye mashimo ya madini, haswa wakati wa usiku.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!