Home » Watu Saba Wakamatwa Nairobi Huku Vita Dhidi Ya Mihadarati Vikiendelea

Watu Saba Wakamatwa Nairobi Huku Vita Dhidi Ya Mihadarati Vikiendelea

Polisi jijini Nairobi wanawashikilia washukiwa saba wanaodaiwa kuhusika na usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya

 

Kulingana na polisi, washukiwa hao walikamatwa katika mtaa wa Huruma jijini humo mwishoni mwa juma wakati wa operesheni iliyoendeshwa na wapelelezi wa kutoka eneo la Starehe.
Zaidi ya kilo 10 za bangi, mizani ya kupimia, jambia na mitungi ya gesi inayoshukiwa kuibiwa zilipatikana wakati wa uvamizi huo wa Jumamosi.

 

Gari lililokuwa likitumika kusambaza shehena hiyo haramu katika maeneo mbalimbali ya jiji pia lilizuiliwa.

 

Washukiwa saba waliotajwa kuwa ni Alex Murimi, Woche Sipa, Clinton Odinga, Kevin Kimani, Mohamed Wako, John Chege na Hassan Yussuf wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka kuanzia kusafirisha dawa za kulevya hadi kukutwa na dawa za kulevya na kujitayarisha kufanya uhalifu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!