Home » Afueni Kwa Kioni Huku Mahakama Ikizuia Mrengo Wa Kanini Kega Wa Jubilee

Afueni Kwa Kioni Huku Mahakama Ikizuia Mrengo Wa Kanini Kega Wa Jubilee

Ni afueni kwa mrengo wa Jubilee unaoongozwa na Jeremiah Kioni baada ya Mahakama ya Kisiasa ya Mizozo ya Vyama vya Kisiasa (PPDT) kutoa maagizo ya kukomesha mrengo unaoongozwa na Kanini Kega kuitisha mikutano yoyote.

 

Katika malalamishi yaliyowasilishwa na Jeremiah Kioni, David Murathe na Kagwe Gichohi, chama cha Jubilee kilielekea PPDT kwa misingi kuwa mrengo wa Kanini Kega umepuuza maagizo ya awali ya mahakama kwamba hali iliyopo idumishwe na hakuna mtu aliyeidhinishwa kutoa mawasiliano kwa niaba ya chama kingine zaidi ya Kioni.

 

Walalamishi waliendelea kudai kuwa walalamikiwa walitoa notisi mbili za kutaka kukiondoa chama hicho kwenye Muungano wa Azimio na kufanya Kongamano la Wajumbe wa Kitaifa (NDC).

 

Walisema notisi hizo mbili ni maamuzi mazito ambayo yana umuhimu mkubwa kwa chama na kwa hivyo inafaa kusubiri hukumu za mahakama ikiwa mrengo wa Kega una mamlaka ya kutoa notisi hizo.

 

Mnamo Juni 13, mrengo wa Kega uliandikia barua Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party, wakitaka kuondolewa kwenye Hati ya Makubaliano inayokifunga kwa muungano huo.

 

Kundi hilo lilisema liliazimia kuondoka Azimio wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichofanyika Juni 6, 2023.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!