Home » Mudavadi Ataka Viongozi Kukumbatia Mswada Wa Fedha

Waziri Mkuu Musalia Mudavadi ametoa wito wa kuwajibika kwa pamoja kuhusu kutoza ushuru na kuwataka viongozi kukumbatia mabadiliko kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mzozo wa kifedha nchini.

 

Akizungumza katika ibada ya kanisa mjini Kakamega Jumapili, Mudavadi amekariri kuwa matatizo yanayokumba Kenya si ya kibinafsi kwa rais, bali ni matatizo ya pamoja kwa watu wa Kenya.

 

Mudavadi amehakikishia mpango wa Kenya Kwanza kuajiri walimu elfu 30,000, akisema haitawezekana ikiwa mapato hayatakusanywa kupitia ushuru.

 

Akiwa bado anazungumzia ushuru, Gavana wa Kakamega Fernandes Baraza ndio gavana wa kwanza wa upinzani ambaye amethibitisha kuunga mkono hatua za serikali.

 

Gavana aliishukuru kamati ya fedha kwa kuchukua maoni ya masuala muhimu yaliyotolewa na umma wakati wa ushirikishwaji wa umma ambao ulisaidia katika marekebisho ya Mswada wa Fedha wa 2023.

 

Baraza amewataka Wabunge kupitisha mswada huo unapoelekea kusomwa kwa mara ya tatu, ili kumsaidia rais kutimiza ajenda za kiuchumi zilizopendekezwa katika manifesto ya Kenya Kwanza.

 

Bunge Jumatano lilipitisha mswada huo huku wabunge 176 wakipiga kura ya NDIYO na 81 wakipiga LA.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!