Home » KRG The Don Kuchukua Jukumu La Kumlipia Karo Yvonne Njoki

KRG The Don Kuchukua Jukumu La Kumlipia Karo Yvonne Njoki

Rapa kutoka Kenya KRG the Don almaarufu Bughaa ameamua kufadhili masomo ya chuo kikuu cha Yvonne.

 

Akizungumza na Nicholas Kioko, KRG aliamua kugharamia masomo ya msichana huyo ili kumsaidia, si kama binti yake, bali kama msichana mdogo mwenye ndoto kubwa.

 

KRG the Don alimpigia simu Yvonne kwenye video ya moja kwa moja na kumwomba atume ratiba na akaunti ya shule.

 

Aliahidi kulipia karo ya shule ya msichana huyo punde tu Yvonne atakapokuwa tayari.

 

KRG alisema wazi kwamba uamuzi na matendo yake yamechochewa na upendo wake kwa Yvonne na watu hawapaswi kuhitimisha kuwa yeye ndiye baba mzazi.

 

Yvonne ni msichana wa miaka 20. Mama yake alidai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na KRG mwaka wa 2002. Anaamini kuwa uhusiano wake na KRG ulisababisha Yvonne kuzaliwa.

 

Hata hivyo, KRG anahisi kwamba mamake Yvonne anamkandamiza binti yake kwa kuwa yeye si baba mzazi.

 

“Mwaka 2002 nilikuwa na umri wa miaka 11, hakuna jinsi mimi ni baba yako, wewe ulizaliwa 2003 hivyo haingiani, mimi nilikuwa darasa la sita mwaka huo, wenzangu wanaweza kushuhudia hilo na mimi sio Nairobi wakati huo.”

 

Krg the Don na anayedaiwa kuwa bintiye Yvonne Njoki

 

Katika mahojiano ya awali, mwanamuziki huyo alisema hatakwenda kupima DNA kwa kuwa ana uhakika kwamba yeye si baba Yvonne na pesa hizo zinaweza kutumika kulipa ada ya shule ya Yvonne badala yake.

 

Yote kwa rapper huyo amechukua jukumu na kuamua kumlipia karo mwanadada huyo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!