Home » Wawakilishi Wadi Watishia Kugoma

Wawakilisi wadi wameipa Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) wiki moja kurekebisha mapendekezo ya mabadiliko ya mishahara yao au waamzishe mgomo katika mabunge ya kaunti kote nchini.

 

Haya yanajiri baada ya SRC, katika waraka wa Jumatano, kuwasiliana na wawakilisi wadi kwamba kuanzia mwezi ujao watapokea Ksh Elfu mia.154,481 kutoka Ksh Elfu mia.144,375.

 

Nyongeza ya mishahara, ambayo itaanzishwa kwa awamu mbili, pia itashuhudia mishahara ya maspika wa mabunge ya Kaunti ikiongezwa hadi Ksh.elfu mia 562,312 kutoka Ksh.elfu mia 525,525 katika mwaka huu wa kifedha lakini kiasi hicho kitapanda hadi Ksh elfu mia.601,674 katika mwaka wa kifedha wa 2024/25. .

 

Manaibu Spika kuanzia Julai mosi watapata Ksh. Efu mia 231,722 kutoka Ksh.Elfu mia 216,563 huku idadi ikitarajiwa kupanda hadi Ksh.Elfu mia 247,943 katika mwaka wa kifedha wa 2024/25 huku viongozi walio wengi na wachache wakipata Ksh.elfu mia 191,324 kuanzia Julai na Ksh. Elfu mia 204,717 kwa mwezi mwaka ujao wa fedha.

 

Wawakilisi wadi wanapinga mapendekezo ya nyongeza ya mishahara kwa misingi kwamba si ya haki kwa sababu maspika wa kaunti, naibu spika, viongozi wengi na walio wachache ndio hasa walionufaika zaidi.

 

Kulingana na Philemon Sabulei, Mwenyekiti wa Baraza la Mabunge ya Kaunti na mwakilishi wadi wa Elgeyo Marakwet, mabunge yote 47 ya kaunti yataahirishwa hadi SRC ifanye marekebisho ya nyongeza ya mishahara.

 

Spika wa Bunge la Kaunti ya Makueni aliongeza kuwa malipo yanafaa kuanza na wajumbe wa Mabunge ya Kaunti na wala sio maspika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!