Home » Mwalimu Bomet Afariki Kwa Kujitoa Uhai

Masomo na shughuli zingine zilitatizwa Usiku wa jana Jumanne katika Shule ya Msingi ya Bukacha katika Kaunti ya Bomet, baada ya mwalimu wa kiume kuingia katika chumba cha mwenzake katika makao ya wafanyikazi na kujiua.

 

Mwili wa marehemu ulikutwa ukining’inia juu ya paa ya chumba cha mwalimu mwenzake.

 

Kulingana na mkuu wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Bomet Mashariki John Karani, marehemu alionekana akiingia katika chumba hicho na hakutoka nje.

 

Karani alisema timu ya maafisa kutoka afisi yake na wale wa idara ya elimu wanafanya uchunguzi ili kubaini ni nini hasa kilifanyika, ikizingatiwa kuwa hakuacha dokezo katika eneo la tukio.

 

Katibu mtendaji wa KNUT tawi la Bomet Malel Langat alisema kuwa marehemu alikuwa mmoja wa walimu waliofaulu kupata uhamisho hadi kaunti ya nyumbani kutoka kaunti jirani ya Narok.

 

Mwili huo umehamishiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Longisa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!