Home » Maafisa 8 Wafariki Lamu Baada Ya Gari Lao Kunyanga Kilipuzi

Maafisa wanane wa Kikosi Maalum cha KDF waliuawa jana Jumanne baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga kilipuzi eneo la Bodhei mpakani mwa kaunti za Lamu na Garissa.

 

Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati askari hao ambao wote walifariki papo hapo walipokuwa wakishika doria katika eneo hilo.

 

Miili ya maafisa walioaga dunia imepatikana lakini utambulisho wao bado haujafahamika kutokana na ukubwa wa mlipuko huo ambao uliripotiwa kuharibu miili yao kiasi cha kutotambulika.

 

Wanajeshi wameshughulikia eneo la tukio na kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.

 

Aidha wakenya kwenye mitandao za kijamii wameanza kulaumu serikali kwa kufungulia mipaka ya Kenya na Somalia huku serikali ikijua uwepo wa wanamgambo wa Al-Shabaab.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!