Manzi Wa Kibera Amuoa Mpenzi Wake Wa Miaka 67
Sosholaiti wa Kenya na video vixen Manzi wa Kibera hayupo sokoni tena.
Wambo almaarufu manzi wa Kibera alifanya harusi na Nzioki mwenye umri wa miaka 67 katika hafla iliyohudhuriwa na marafiki wa karibu.
Video vixen alikuwa amevalia gauni jeupe la harusi huku Mzee akiwa amevalia suruali nyeusi na kanzu nyekundu.
Wambo alisambaza picha za harusi yao kwenye mitandao ya kijamii na kuongeza kuwa haijalishi unampenda nani mradi tu uwe na furaha.
Wawili hao hivi majuzi walitangaza kuwa wamerudiana baada ya kutengana hadharani katika mahojiano na Nicholas Kioko, Mzee alisema wambo alirudisha hati yake ya umiliki na wawili hao wakakubaliana kurekebisha mambo na kurudiana.
Wakati wa mahojiano, sosholaiti huyo alipiga magoti na kuomba msamaha kwa kumweka mpenzi wake katika mambo mengi na kumwacha alipomhitaji.
Wawili hao pia walitangaza waziwazi mapenzi yao na kutupilia mbali madai ya kutaka kujitangaza.
Katika mahojiano ya awali, Manzi Wa Kibera alisema walikutana mwaka wa 2022. Alieleza kuwa mwanamume huyo amekuwa mjane tangu kifo cha mkewe mwaka wa 2007.
Kwa upande wake Mzee alisema Manzi Wa Kibera si mdogo sana kwake kwani ana uwezo wa kumtunza, tofauti na vijana wa kiume.
“Yeye si mdogo kwangu, naweza kumtunza na kutimiza ahadi zangu tofauti na vijana ambao wako hapa nje wakivunja mioyo ya wasichana.”
Wawili hao wana mipango ya kujenga nyumba pamoja na kuanzisha familia.