Home » Naibu Spika Wa Kiambu Akamatwa Kwa Madai Ya Ufisadi

Naibu Spika wa Kaunti ya Kiambu John Njue Njiru ambaye pia ni mwakilishi wadi wa Wadi ya Hospitali ya Thika amekamatwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC).

 

Kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha EACC Integrity Center ambapo anarekodi taarifa.

 

Mshukiwa anadaiwa kudai hongo ya Kes.130,000 na sehemu ya bure ya ardhi ya mlalamishi ndani ya mji wa Thika ili kuwezesha mlalamishi aruhusiwe kuendelea na shughuli zozote kwenye ardhi yake yenye thamani ya Kes.15Milioni ndani ya Mji wa Thika.

 

Ikumbukwe kwamba visa vya maafisa wa serikali kujihusisha katika ufisadi vimeendelea kukithiri zaidi siku za hivi karibuni wakenya wengi wakiisuta serikali kwa kutoingilia kati suala hili kwa kina na kukomesha visa hii.

 

Kadhalika wakenya walikaribisha hatua ya mbunge wa Thika Alice Ng’ang’a ya kurudisha adhabu ya kinyongo kwa wale wataojihusisha na ufisadi nchini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!