Home » Moses Kuria Aweka Kiwango Kipya Cha Bei Ya Mvinyo Wa 250ml

Waziri wa Biashara na Uwekezaji Moses Kuria ametoa uamuzi kwa wauzaji na watengenezaji wote wa pombe na kuweka kiwango kipya cha bei ya mvinyo na vinywaji vikali kuwa Ksh250.

 

Akizungumza huko Tharaka Nithi, Kuria amesema kuwa yeyote atakayepatikana akiuza chupa ya mililita mia 250 ya pombe chini ya kiwango cha bei ya shilingi mia 250 atachukuliwa kuwa mshukiwa na atakamatwa mara moja.

 

Waziri huyo amebaini kuwa alikuwa ametoa pendekezo kwa Kamati ya Fedha ya Bunge la Kitaifa ambalo litahakikisha kwamba sheria hiyo inatekelezwa ipasavyo.

 

Waziri huyo ameeleza kuwa bei hiyo haipaswi kuwa chini ya Ksh250 kwa sababu ya gharama za ziada zikiwemo stempu za ushuru alizoeleza kwa kina.

 

Aidha, amebainisha kuwa ununuzi wa stempu hizo ulikuwa wa malipo ya awali na hivyo wapo wanaouza kwa bei nafuu walijihusisha na vitendo visivyo halali ikiwemo matumizi ya stempu feki.

 

Kwa watumiaji ambao watafikiri kwamba kiasi hicho kilikuwa ghali sana, Kuria amewataka kutumia vinywaji vingine ikiwa ni pamoja na maziwa na kuongeza kuwa orodha ya bei mpya itachapishwa mara kwa mara.

 

Zaidi ya hayo, amebainisha kuwa serikali itaongeza ufadhili kwa wa shirika la Kampeni ya Kitaifa Dhidi ya Utumizi Mbaya wa Dawa za Kulevya (NACADA) ili kupatikana ufanisi katika vita dhidi ya matumizi mabaya ya pombe nchini, haswa miongoni mwa vijana.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!