Home » Wizara Ya Afya Yatupilia Mbali Uvumi Wa Wimbi Jipya La Korona

Wizara Ya Afya Yatupilia Mbali Uvumi Wa Wimbi Jipya La Korona

Wizara ya Afya imetupilia mbali ripoti za wimbi jipya la ugonjwa wa korona nchini.

 

Katika taarifa, waziri wa Afya Susan Nakhumicha amesema nchi inakabiliwa na kuongezeka kwa homa kutokana na msimu wa baridi.

 

Aidha amewataka wakenya kuchukua tahadhari dhidi ya homa hiyo Kutokana na ufuatiliaji wa wizara ya afya, hamna ongezeko la korona huku akiwarai wananchi kuripoti visa vyovyote vilivyo na dalili sawa na korona

 

Hata hivyo amewahimiza wananchi kuwa ni vyema tukajikinga na homa hiyo na kusistiza kuwa kuna chanjo ya homa ambayo inaweza kutolewa katika vituo vingi vya matibabu.

 

Waziri huyo amemtaka yeyote aliye na homa ya mafua kujilinda kwa kuvaa barakoa, kujisafisha na kuepuka kugusa sehemu za mdomo na pua.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!