Home » Mbunge Wa Ugenya Alaumu NHIF

Mbunge wa Ugenya David Ochieng’ ameitaja Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF) kama taasisi fisadi kutokana na kushindwa kulipa bili mara kwa mara kwa watu wanaopokea matibabu hospitalini.

 

Akizungumza katika runinga moja humu nchini, mbunge huyo ameelezea masikitiko yake kuhusu huduma ambazo NHIF inawapa wananchi na hata kudai kuwa anaweza kufutilia mbali hazina hiyo na kuweka huduma ya bima iwapo angekuwa rais wa nchi.

 

Mbunge huyo wa Ugenya ameshutumu serikali kwa kusimamia vibaya sekta ya afya na alitumai kuwa utawala wa Kenya Kwanza ungetatua masuala yanayohusu NHIF, NSSF na sekta ya afya kwa jumla.

Ameongeza kuwa fedha zinazopokelewa kwa ajili ya afya zinapaswa kutumwa kwa afya ili kuzuia matumizi mabaya ya fedha.

 

Aidha, hivi majuzi wengi wa wakenya wanahisi NHIF haisadii walivyotarajia kwani hosptali nyingi zilihitaji pesa za ada ambazo walishindwa kutoa wakati wa matibabu wakijua NHIF ingesimamia kila kitu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!