Home » ‘Nakuchukia!’ Paula Kajala Amlipua Harmonize
Paula Kajala and Harmonize

Paula Kajala and Harmonize

Mwanamitindo Paula Kajala ambaye ni mtoto wa muigizaji mkongwe Fridah Kajala Masanja amefunguka kuwa ni kweli Harmonize alifanya jitihada za kumtongoza kipindi hicho akiwa pia na mama yake mzazi.

 

Akiongea kwenye kipindi cha Beyond the Gram kinachorushwa moja kwa moja na Emerald TV, Paula alisema anamchukia Harmonize kwa roho yake yote.

 

Mrembo huyo ambaye wiki iliyopita alimtaka babake kuacha kufuatilia maisha yake, safari hii alielekeza hasira zake kwa Konde Boy akisema anamchukia mwanamuziki huyo.

 

Paula alisema kuwa watu wa nje na mbali na yeye na mama yake wanadhani kuwa hawana mipaka na ndiyo maana Harmonize aliteleza kwenye ganda hilo la ndizi akijaribu kuwapata Paula na mama yake.

 

“Kwa sababu watu wa nje wanahisi hatuna mipaka, na ndiyo maana mtu wa aina ya Harmonize anathubutu kunitongoza ingawa alikuwa mpenzi wa mama yangu, namchukia,” Paula alisema kwa sehemu.

 

Mnamo 2021, picha na jumbe za kutongoza zilivuja ambazo zilidaiwa kutoka kwa Harmonize kuelekea kwa Paula, wakati alikuwa akitoka na mama yake.

 

Tukio hilo lilimfanya Kajala kuvunja uhusiano wake na Harmonize kwa hasira lakini baada ya mwaka mmoja msanii huyo wa kundi la Konde Gang kujutia kitendo cha kumtumia picha chafu Paula na kuomba radhi huku akimtaka Kajala kurudiana naye.

 

Hatimaye Juni mwaka jana, Kajala alikubali kumsamehe Harmonize na wakarudiana, kwenye hafla maalum Milimani City.

 

Lakini baada ya miezi sita zaidi wawili hao walitengana na kipindi hicho kukazuka tetesi kutoka kwa wanamtandao kuwa Harmonize alikuwa analala kitanda kimoja na Kajala na bintiye huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai kuwa Harmonize ndiye alimfungulia duka la nguo Paula. .

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!