Kenya Na Djibouti Zatia Saini Mkataba Wa Maelewano
Kenya na Djibouti zimetia saini hati nne za maelewano kuhusu maeneo tofauti kwa lengo la kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Katika taarifa, mataifa hayo mawili yametia saini Mkataba wa kuwezesha ushirikiano katika nyanja ya maendeleo ya nishati.
Makubaliano hayo yanahusu kushiriki ujuzi wa kiufundi, mbinu, uzoefu,nyaraka, maarifa na nyenzo kati ya wahusika kupitia ushirikishwaji wa pande zote, unaozingatia maendeleo ya jotoardhi.
Akiongea wakati wa kutia saini Djibouti, Rais William Ruto alisema Sambamba na hilo, alimshukuru mwenzake rais Omar Guelleh, kwa kuharakisha mchakato wa mazungumzo, kuwezesha uanzishwaji wa miundombinu na vifaa muhimu, na kuanzisha utekelezaji wa mradi unaopendekezwa wa Hanle Garabbayyis.
Chini ya mradi huo, Kampuni ya Kuzalisha Umeme Kenya (KENGEN) itachimba visima viwili vya jotoardhi nchini Djibouti.
Rais Ruto amebainisha kuwa KENGEN tayari imetimiza awamu ya kwanza ya mkataba na Ofisi ya Djiboutien De Development De Energie Geothermique (ODDEG) na kufanikiwa kuchimba kisima kimoja cha jotoardhi katika awamu ya awali ya mradi wa Galla Le Koma.
Kenya na Djibouti pia zimetia saini Mkataba wa Ushirikiano wa Kiufundi katika Maendeleo ya Masuala ya Vijana na Sanaa, ambao unaanzisha mfumo wa ushirikiano katika uundaji wa vifaa vya kisasa katika nyanja za michezo na sanaa.
Zaidi ya hayo, nchi hizo mbili zitakuwa na ushirikiano wa pamoja katika Chuo cha Huduma za Kigeni.
Mashauriano ya mara kwa mara na ushirikiano katika maeneo ya elimu na kisayansi yatafanywa ndani ya mfumo wa shughuli za programu zilizokubaliwa.
Mkataba huu utaimarisha mabadilishano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, kukuza maendeleo endelevu ya utalii, na kuimarisha utalii.