Home » Hazina Ya Kitaifa Yatoa Pesa Kwa Kaunti
National treasury

Jengo la hazina ya kitaifa

Hazina ya Kitaifa imetoa Ksh.33 bilioni zinazodaiwa na kaunti ili kulipa bili mbalimbali ambazo hazijakamilika.

 

Kati ya pesa hizo, Ksh.10 bilioni zimegawiwa kwa Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Serikali-Maeneobunge (NG-CDF).

 

Katibu Mkuu wa Hazina ya Kitaifa Chris Kiptoo alisema fedha hizo, kutoka kwa mgao sawa wa mapato wa Aprili, zitawezesha kaunti kutoa huduma muhimu kwa wapiga kura wao.

 

Haya yanajiri takriban mwezi mmoja baada ya Baraza la Magavana (CoG) kutishia kuzima kaunti kutokana na kucheleweshwa kwa ugawaji wa hisa sawa na Hazina ya Kitaifa.

 

Akizungumza mwezi wa Mei, Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa, ambaye anahudumu kama mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya baraza la magavana, alisema Hazina ya Kitaifa inadaiwa Ksh.94.3 bilioni kwa miezi ya Machi hadi Mei 2023.

 

Aidha, alibainisha kuwa kuchelewa kutolewa kwa fedha hizo kulilemaza utoaji wa huduma na kusababisha mateso makubwa kwa watumishi wa kaunti ambao walikaa kwa miezi kadhaa bila malipo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!