Home » ‘Hakuna Mgogoro’: Waziri Machogu Asema Serikali Imetoa Fedha Kwa Shule

‘Hakuna Mgogoro’: Waziri Machogu Asema Serikali Imetoa Fedha Kwa Shule

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anasema hakuna shida katika taasisi za masomo kote nchini kufuatia ripoti za kucheleweshwa kwa malipo ya masomo.

 

Akiongea na runinga moja humu nchini, Waziri Machogu amethibitisha kuwa Wizara ya Elimu imepokea fedha kutoka kwa Hazina ya Kitaifa na imeanza usambazaji wake kwa shule za msingi, sekondari na zile za sekondari za msingi kote nchini, na kuahidi kuwa pesa hizo zitaingia kwenye akaunti ya shule kati ya wikendi hii na wiki ijayo.

 

Hii ni kufuatia ukaguzi wa mara kwa mara katika kaunti za Kajiado, Kisii, Nyamira, Siaya na Mombasa ilibaini kuwa shule mbalimbali bado hazijapokea pesa hizo kufikia kufungwa kwa shughuli zake jana Ijumaa.

 

Katika kile kilichoonekana kuashiria mwisho wa kusubiri kwa muda mrefu kwa shule kote nchini, serikali ilikuwa Alhamisi imetangaza mipango ya kufadhili wanafunzi kwa shule za msingi, sekondari na za upili nchini kote kufikia Juni 9, 2023.

 

Wengi wa wakuu wa shule wamekuwa wakilalamikia ugumu wa kuendesha shughuli za shule kwenye hazina tupu, madai ambayo wazirianakanusha.

 

Alipokuwa akijibu maswali ya Wabunge Jumatano, Waziri Machogu alikuwa amedokeza kuwa shule zilipaswa kupokea Ksh.28 bilioni lakini mnamo Alhamisi uchanganuzi wa Hazina ya Kitaifa ulionyesha kuwa shule zinatarajiwa kupata Ksh.24 bilioni pekee.

 

Aidha Wakuu hao wa shule pia wanahoji vigezo ambavyo wizara ilipitisha katika kutoa fedha hizo kwani inatarajiwa kutoa asilimia 50 ya wanafunzi katika muhula wa kwanza, asilimia 30 muhula wa pili na asilimia 20 muhula wa tatu.

 

Waziri Machogu alisema kuwa utekelezaji wa mkakati huu ni sehemu ya mageuzi ambayo bado yanaendelea.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!