Home » Rais Ruto Kuondoka Nchini Kuelekea Zambia

Rais William Ruto anatarajiwa kuondoka nchini leo kuhudhuria Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa COMESA mjini Lusaka, Zambia.

 

Kwa mujibu wa Msemaji wa Ikulu, Hussein Mohamed lengo la Mkutano huo litakuwa katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama wa COMESA.

 

 

Zaidi ya hayo, Wakuu wa Nchi watajadili hali ya sasa ya eneo la COMESA, pamoja na masuala yanayohusu amani na usalama.

 

Rais ruto anaondoka nchini kukiwa na hali ya mkanganyiko wa mswaada wa fedha 2023 ambapo hiyo jana kumekuwepo na ishara zote kwamba wabunge ambao ni wengi wa Kenya kwanza watapitisha mswaada huo.

 

Yakijiri hayo kinara wa upinzani Raila Odinga vile vile anatarajwia kutoa tangazo lake hii leo kuhusiana na msimamo wa upinzani kwa mustabali wa siasa kwa sasa macho yote yameelekezwa bunge kuona jinsi mswaada utakapoidhinishwa au kuungushwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!