Home » Mzee Amlilia Manzi Wa Kibera
Manzi Wa Kibera and ex lover

Manzi wa Kibera with her lovely teddy bear Photo courtesy.

Sosholaiti Sheriffa Wambui almaarufu Manzi Wa Kibera aliachana na mpenziwe mzee mwishoni mwa Mei 2023, kabla ya harusi yao iliyopangwa.

 

Akiongea wakati wa mahojiano na MwanaYouTube Nicholas Kioko, mzee huyo alisema kuwa Manzi wa Kibera alimwacha baada ya kupata pesa.

 

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 66 alisema sosholaiti huyo amemgadhabisha kabisa, akikataa kupokea simu zake anapojaribu kuwasiliana naye.

 

“Amenitoroka akanitia wasiwasi sana. Vile nilikua nakaa mbeleni si vile nko dakika hii. Nikipiga simu kwake ata hachukui. Alikua anaona nko na kapesa, akaona kapesa kameisha,” alisema.

 

Mzee huyo alizidi kulalamika kuwa Manzi wa Kibera alitoroka na hati umiliki yake ya shamba “tittle deed”.

 

“Ata kuna title yangu nilimpatia ya shamba. Ilikua tujenge kanyumba hapo tukue tunakaa hapo na yeye tukipata kakitu kidogo tulime, tupate ata kama ni mbuzi tufuge. Nilimpatia aniwekee. Nataka anirudishie kama inawezekana. Kama anaona hatuendelei anaweza kunirushia title yangu,” alisema

 

‘Alichukua simu ya kwanza, wakati niliongea pahali ya title hakupiga simu tena na hakuchukua simu tena. Ata nkimpigia hachukui,”alisema

 

Mzee huyo alizidi kumsihi Manzi wa Kibera amrudishie hati yake ya umiliki, akisema yuko tayari kumsamehe ili wakae katika shamba lao.

 

“Manzi wa Kibera nasema kama unanipenda niletee title deed yangu. Kama unaona hatukai pamoja ulete. Na kama unaona tunakaa pamoja ulete title yangu ndo tujue vile tutapanga kujenga kanyumba huko nyumbani tukue tunalimalima huko tuachane na pande ya town huko.

 

Namwambia hivo tu,alisema mzee huyo pia alijiamini kuwa bado anaweza kumshawishi Manzi wa Kibera warudiane naye ili wafunge ndoa.

 

“Namuomba kama anaweza kuja tumalize harusi yetu Na ukimaliza harusi akuache tena? Unajua tukiwa pamoja hatuwezi fanya harusi aniwache

 

“Mzee huonangi ni kama unachezwa Naonanga ni kama kalikua ni kamchezo lakini sikuelewa vizuri kale kamchezo kalikua ndani hapo.

 

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 66 alipendekeza kwa Manzi wa Kibera katika uwanja wa China Square mnamo Aprili 2023 ili sosholaiti huyo amtupie siku chache baadaye.

 

Kumbuka kuwa Manzi wa Kibera anasifika kwa kuwa kwenye mahusiano ya muda mfupi. Hapo awali alikuwa ameolewa na Obidan Dela – kwa wiki mbili fupi sana.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!