Home » Ichung’wah Adai Kuombea Upinzani

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah amefichua kwamba huwaombea vinara wenza wa upinzani kila siku.

 

Akizungumza Bungeni wakati wa shughuli za Bunge Jumanne, Ichung’wah amesema ataendelea kuwaombea viongozi wa upinzani.

 

“Ninataka kuwahimiza Wakenya kuombeana kama vile kila siku ninavyomuombea aliyekuwa Waziri Mkuu (Raila Odinga) na rafiki yangu wa karibu Kalonzo Musyoka. Kila siku mimi hufanya hivyo,” alisema.

 

Amewaalika wawili hao kwenye mkutano wa kesho wa Kiamsha kinywa cha Kitaifa cha Maombi ya Kitaifa mnamo Juni 7, na kuongeza kuwa katika mkutano huo watakaoamua kutohudhuria bado watashirikishwa katika maombi.

 

Pia amesema anawaombea Rais William Ruto, naibu wake Rigathi Gachagua na viongozi wengine wote waliochaguliwa.

 

Ichung’wah ameelezea matumaini kuwa maombi hayo yatasaidia kuwapatanisha Wakenya na kulainisha mioyo ya viongozi wa kisiasa.

 

Kauli yake inajiri muda mfupi baada ya uongozi wa Azimio kutangaza kutoshiriki mkutano huo katika Hoteli ya Safari Park kwa sababu ya ukosefu wa uaminifu.

 

“Ikiwa matukio ya zamani ambapo tulishiriki majukwaa na Kenya Kwanza yatatumika kama mwongozo, Azimio inasadiki kwamba mkutano huo wa Maombi hautoi mazingira ambayo nchi inahitaji kwa unyenyekevu mbele ya Mungu, uaminifu kwa raia na heshima kati ya viongozi,” taarifa inasomeka.

 

“Badala yake, tukio hilo litamvunjia heshima Mungu na nchi kwa maonyesho ya majivuno, vita vya ubora, matumaini ya uongo kwa raia na nyadhifa za uwongo hata kupotosha na kutafsiri nia na viongozi mashuhuri wa Kenya Kwanza. Kwa hivyo tunakataa mwaliko wa kiamsha kinywa.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!