Home » Hinga: Ukifutwa Kazi Pesa Zako Zitakaa Pale Mpaka Ustaafu

Hinga: Ukifutwa Kazi Pesa Zako Zitakaa Pale Mpaka Ustaafu

Katibu Mkuu wa Idara ya makazi na Maendeleo ya Mijini Charles Hinga hii leo Jumanne amefika mbele ya Kamati ya Fedha ya Bunge ambapo ameendelea na utetezi wake kuhusu ushuru wa lazima wa nyumba yenye sambamba na ule uliopo kwenye mswaada tata wa fedha wa 2023.

 

Hinga aliulizwa juu ya mpango wa makazi wa serikali ambao umepata upinzani mkubwa na kuendeleaa kuelezea zaidi kuhusu manufaa huku akiwasuta viongozi walioiingiza siasa katika suala hilo.

 

Kuhusu utendakazi wake, Hinga amesema pendekezo hilo linatofautiana na makazi ya sasa ikizingatiwa kuwa jambo hilo likitekelezwa na hakutakuwa na ushuru wakati wa kujitoa baada ya kustaafu.

 

Kulingana na Hinga michango ya mtu binafsi itabaki bila kutumika hadi mtu atakapostaafu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!