Home » Wakuu Wa Azimio Kuruka Mkutano Wa Maombi ya Kitaifa

Uongozi wa muungano Azimio la Umoja One-Kenya hautashiriki mkutano wa Kiamsha kinywa cha mwaka huu cha Maombi ya Kitaifa kilichoratibiwa kufanyika hapo kesho, tarehe 7 Juni, 2023.

 

Katika taarifa hii leo Jumanne, chama hicho kimethibitisha kwamba uongozi wake ulipokea mwaliko wa hafla hiyo lakini hautashiriki maombi hayo .

 

Spika wa bunge la kitaifa Moses Wtangula mnamo Mei 4 alisema kwamba zaidi ya wageni 2,500 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wa Kitaifakwa ajili ya Maombi ya Mwaka huu, utakachofanyika katika Hoteli ya Safari Park jijini Nairobi kaulimbiu ikiwa ni ‘Upatanisho na Mungu na Mwanadamu’.

 

Katika kukataa mwaliko huo, Azimio imeteta kuwa kifungua kinywa cha maombi hakitoi jukwaa la mazungumzo ya ukweli na ya kijasiri na Wakenya katika kushughulikia masuala muhimu yanayokabili nchi.

 

Wakati wa kikao Bungeni, kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Opiyo Wandayi alisema wabunge wote wa Azimio watahudhuria hafla hiyo.

 

Hata hivyo, alisema kuwa uongozi wa Azimio utashirikishwa mahali pengine na hivyo hautahudhuria maombi hayo.

 

Ikumbukwa Odinga jana alisema kuwa Upinzani watatoa taarifa Alhamisi ya kina kuelezea Wakenya kwa nini wanapinga mswada huo ambao umeibua mjadala mkali nchini.

 

Jumapili, Rais William Ruto alionya wabunge wa Kenya Kwanza watakaothubutu kupinga mswada huo kuwa wataadhibiwa.

 

Naye Odinga jana aliwataka Wakenya kupambana na wabunge wao watakaounga mkono Mswada huo aliosema unalenga kukandamiza raia.
Awali, kiongozi huyo wa Upinzani alikuwa ametoa makataa ya hadi Jumatatu kwa Rais Ruto kufanyia marekebisho Mswada huo la sivyo atangaze maandamano.

 

Mswada wa Fedha wa 2023 unapendekeza kupandishwa kwa ushuru wa bidhaa muhimu kama vile mafuta na kukata wafanyakazi asilimia 3 ya mishahara yao kwa ajili ya mradi wa nyumba.

 

Jana, Rais Ruto alijipata pabaya baada ya waandamanaji kukusanyika nje ya ukumbi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Makazi (UN Habitat) mtaani Gigiri, Nairobi, wakipinga makato ya nyumba.

 

Kiongozi wa Nchi alisalia kimya alipowaona waandamanaji hao waliokuwa na mabango yaliyoandikwa: ‘Usilazimishie Wakenya ushuru wa nyumba’ na kisha kuondoka.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!